KAMA UNATARAJIA KUOA AU KUOLEWA USIFANYE MAKOSA, VINGINEVYO NI BORA UKAENDELEA KU -ENJOY KUWA SINGLE.
Kama unatarajia kuoa au kuolewa usifanye makosa. Vinginevyo ni bora ukaendelea ku-enjoy kua single.
Kama kuna kitu ambacho kinaweza kikakupa pressure, vidonda vya tumbo na ukafirisika kiuchumi na kiakili ama kufa mapema ni wrong marriage yaani ndoa isiyo sahihi.
Mhandisi yeyote yule atakwambia kwamba endapo vitu viwili vilivyoungana vikiwa katika mwendokasi wakati haviendani, uwezekano wa kitu kimoja au vyote kuvunjika ni mkubwa sana.
Ni vema zaidi ukaendelea kuwa single maana haijawahi kutokea mtu akaugua vidonda vya tumbo, pressure, kisukari kwa sababu yupo single... ila waliopo kwenye ndoa zisizo sahihi wanafahamu maumivu wanayougulia.
Kama hakuna upendo urafiki hautakuwepo, tendo la ndoa ni kubakana tu. Ni watoto ndio wanaowafanya waendelee na ndoa. Busara kubwa inahitajika katika kutafuta life partner.
No comments